IQNA

Ongezeko la asilimia 20 la Misahafu inayochapishwa nchini Iran

17:44 - June 23, 2021
Habari ID: 3474034
TEHRAN (IQNA)- Kumekuwa na ongezeko la asilimi 20 la Misahafu iliyochapishwa nchini Iran katika mwaka huu wa Kiirani wa Hijria Shamsia ulioanza Machi 21.

Kwa mujibu wa Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Darul Qur'an Karim la Iran kumekuwa na ongezeko la asilimia 20 la uchapishaji Misahafu au Nakala za Qur'ani Tukufu ikilinganishwa na wakati mshabaha mwaka jana.

Katika mahojiano na IQNA,  amesema vibali 88 vimepewa mashirika mbali mbali kuchapisha misahafu mwaka huu.

Shirika la Darul Qur'an Karim linafungamana na Shirika la Ustawi wa Kiislamu Iran na huwa na jukumu la kusimamisha uchapishaji nakala za Qur'ani nchini Iran.

3979374

captcha