IQNA

Jumuiya ya kupinga uhusiano na Israel yaanzishwa Sudan

20:10 - June 21, 2021
Habari ID: 3474028
Vijana wa Sudan wameanzisha Jumuiya ya Kuunga Mkono Msikiti wa Al Aqsa na Kupinga Uanzishwaji Uhusiano wa Kawaida na Utawala wa Kizayuni wa Israel.

Jumuiya hiyo inapanga kutekeleza shughuli zake kupitia mikakati ya kijamii na kuandaa maandamano ya kupinga hatua ya serikali ya Sudan kuanzisha uhusiano na utawala haramuwa Israel

Kunda idadi kubwa ya watu wa Sudan, hasa vijana ambao wanapinga vikali uamuzi wa serikali ya mpito nchini humo kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel na hivyo jumuiya hiyo inatazamiwa kuwaunganisha wote wanaopinga uhusiano huo.

Tarehe 23 ya mwezi uliopita wa Oktoba, Wizara ya Mambo ya nje ya Sudan ilitangaza kuwa serikali ya mpito ya nchi hiyo imeafiki kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel na hivyo kuifanya Sudan nchi ya tano baada ya Misri (1979), Jordan (1994), Imarati na Bahrain (2020) kufikia mapatano na Israel na kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo wa Kizayuni. Baada ya Sudan, Morocco nayo ilitangaza kuanzisha  uhusiano na utawala huo bandia wa Israel

Kufuatia kutangazwa uamuzi wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel, makundi mbalimbali ya kisiasa nchini Sudan yamepinga vikali makubaliano hayo, vikiwemo vyama washirika katika muungano unaotawala nchi hiyo.

Miezi kadhaa baada ya kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel kama njia ya kujikurubisha kwa Marekani na kupata misaada ya kifedha ya nchi hiyo, serikali ya Sudan imeeleza kuvunjwa moyo na matokeo ya hatua hiyo baada ya kunyimwa misaada hiyo.

3979130/

Kishikizo: sudan israel
captcha