IQNA

Kiongozi Muadhamu

Wananchi wa Iran ndio washindi wakuu wa uchaguzi

19:01 - June 19, 2021
Habari ID: 3474021
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amepongeza hatua ya kujitokeza kwa wingi wananchi wa Iran katika uchaguzi mkuu wa jana Ijumaa na kusisitiza kuwa, 'washindi wakuu wa uchaguzi ni wananchi wenyewe, ambao azma yao thabiti haikuvunjwa moyo na ama janga (la Corona) au njama za kuwakatisha tamaa.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo katika ujumbe wake kwa taifa la Iran, kufuatia kumalizika kwa amani Uchaguzi wa Urais wa Jamhuri ya Kiislamu, ambapo amewashukuru na kuwapongeza sana wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo la jana Ijumaa.

Kiongozi Muadhamu amesema, kujitokeza kwa hamasa na idadi kubwa wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika uchaguzi huo kumeongeza ukurasa mwingine wenye kung'aa kwenye (rekodi) ya hadhi na heshima yao.

Ayatullah Ali Khamenei amebainisha kuwa, mandhari ya kupendeza ya mijumuiko ya watu katika vituo vya kupigia kura hapo jana ni ishara ya wazi ya azma thabiti, moyo wenye matumaini na kuwa macho wananchi wa Iran ya Kiislamu.

Amesema hata propaganda za maadui wa Jamhuri ya Kiislamu hazikuwakatisha moyo wananchi wa Iran, ambao wamejitokeza kwa wingi mno kupiga kura.

Kadhalika Kiongozi Muadhamu amevipongeza vyombo vya uchaguzi na vya usalama kwa kuendesha na kusimamia vizuri mchakato na zoezi zima la uchaguzi huo.

Katika ujumbe wake huo, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametoa mwito kwa Rais-mteule, na viongozi waliochaguliwa wa mabaraza ya Kiislamu ya miji na vijiji kuchapa kazi na kulihudumia taifa la Iran kwa dhati na moyo mmoja.

3474985/

captcha