IQNA

Tovuti kubwa zaidi ya kupakua tilawa ya Qur'ani duniani kwa lugha 21

12:36 - June 09, 2021
Habari ID: 3473991
TEHRAN (IQNA) – Mp3Quran ni tovuti kubwa zaidi ya kupakua au kudownload tilawa ya Qur'ani Tukufu ya wasomaji mbali mbali duniani.

Tovuti hiyo ya https://www.mp3quran.net/sw ina sauti ya  tilawa za zamani na za sasa za wasomaji wa zamani na wa sasa wa Qur'ani Tukufu.

Majina ya wasomaji au maqarii yamepangwa kwa alfabeti ili kumrahisishia mtafutaji uwezo wa kupata qarii amtakaye.

Tovuti hii ina lugha 21 kama vile Kiswahili, Kiingereza, Kiarabu, Kifarsii, Kichina, Kihausa, Kijerumani n.k.

3976249

Kishikizo: tovuti qurani tukufu
captcha