IQNA

Sheikh Issa Qassim

Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ndio chanzo cha kuundwa harakati za mapambano Kiislamu

11:41 - June 04, 2021
Habari ID: 3473978
TEHRAN (IQNA)- Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Bahrain amesema moja kati ya mafanikio makubwa zaidi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ni kuundwa mrengo wa muqawama au harakati za mapambano ya Kiislamu na kupata ushindi mrengo huo katika mapambando dhidi ya mfumo wa kibeberu.

Sheikh Issa Qassim, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu nchini Bahrian ameyasema hayo Alhamisi alipohutubu katika Kongamano la Kimataifa la 'Imam Khomeini na Ulimwengu wa Kisasa"ambao limefanyika katika Haram Takatifu ya Imam Khomeini (MA) muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mjini Tehran. Ameongeza kuwa, Mapinduzi ya Kiislamu yaliweza kuibua fikra za Kiislamu katika taifa la Iran na kisha katika umma wa Kiislamu duniani na matokeo ya hilo ni kuundwa mrengo wa Mapambano ya Kiislamu.

Akihutubukwa njia ya video katika semina hiyo, Sheikh Issa Qassim amesema leo mhimili wa muqawama unasimama kidete na kwa nguvu zote dhidi ya mradi wa kuanzisha uhusiano na adui Muisraeli. Amesema mradi huo wa kuzishawishi nchi za Kiarabu na Kiislamu zianzishe uhusiano na utawala haramu wa Israel unalenga kuvuruga umma wa Kiislamu. Aidha amesema kusimama kidete huko pia ni kati ya mafanikio makubwa ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Bahrain amekumbusha kuwa, mhimili wa muqawama unajumuisha watu ambao ni watiifu kwa umma wa Kiislamu na ambao ni kutoka kaumu, madhehebu na lugha mbali mbali ambapo Iran ya Kiislamu iko katika mstari wa mbele wa harakati zote za mhimili wa muqawama au mapambano ya Kiislamu.

/3975345

captcha