IQNA

Sayyid Nasrallah:

Marekani ndio utawala dhalimu zaidi duniani

19:28 - July 08, 2020
Habari ID: 3472941
TEHRAN (IQNA) - Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Marekani ndio utawala dhalimu zaidi duniani na chokochoko zote zilizofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Lebanon zimefanyika kwa uungaji mkono wa Washington.

Sayyid Hassan Nasrallah ameyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kupitia kanali ya televisheni ya Al-Manar, ambapo aliihutubu serikali ya Marekani kwa kusema, "sera yenu ya kuwabana wananchi wa Lebanon haitakuwa na matokeo mengine ghairi ya kuipa nguvu zaidi Hizbullah na kudhoofisha ushawishi wenu na vibaraka wenu."

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kupiga hatua za maendeleo na ustawi licha ya vikwazo na mashinikizo ya maadui.  Sayyid Nasrallah ameashiria kuhusu ushindi mtawalia wa kambi ya muqawama na kufeli njama za Marekani nchini Lebanon na katika eneo la Asia Magharibi mwa ujumla.

Amelipongeza taifa la Iran kwa kusimama kidete mkabala wa mashinikizo na vikwazo vya maadui hususan Marekani na kueleza bayana kuwa, "mfumo unaoiongoza Iran umejitosheleza, kwa nini mnaouogopa huu mfumo? Iran iko tayari kuiuzia Lebanon mafuta kwa kutumia sarafu ya pauni ya Lebanon."

Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema balozi wa Marekani nchini humo amekuwa akiingilia wazi wazi masuala ya ndani ya nchi hiyo na kwamba nchi hiyo ya Kiarabu inapinga vikali tabia hiyo. Amemhutubu balozi huyo, Dorothy Shea kwa kumwambia: Marekani haina ustahiki wa kuyapa somo mataifa mengine kuhusu haki za binadamu wakati dola hilo la kibeberu ni mkiukaji nambari moja wa haki hizo, mbali na kuunga mkono na kufadhili ugaidi katika eneo. 

3471927

captcha