IQNA

Msomi wa Iran

Taasisi za utafiti Marekani hupanga sera dhidi ya harakati za mapambano ya Kiislamu

12:31 - July 08, 2020
Habari ID: 3472940
TEHRAN (IQNA) – Msomi wa Iran Dkt. Hakimeh Saghaye-Biria, amesema taasisi za utafiti nchini Marekanizinatumiwa kupanga sera za serikali ya nchi hiyo kuhusu ulimwengu wa Kiislamuna hasa dhidi ya harakati za muqawama au mapambano ya Kiislamu.

Dkt. Saghayeh-Biria ameyabainisha hayo katika kitabu chake alichokiandika chenye anuani ya "Chuki dhidi ya Kiislamu ya Kisiasa katika Taasisi za Utafiti Marekani: Kukabiliana na Nguvu za Harakati ya Mapambano ya Kiislamu" (Political Islamophobia at American Institutes: Battling the Power of Islamic   Resistance).

Dkt. Saghayeh-Biria ni msomi wa historia, ustaarabu na mapinduzi ya Kiislamu katika Kitivo cha Fikra za Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Tehran.

Kitabu hicho kimezinduliwa Jumatatu 6 Julai mjini Tehran katika kikao kilichofanyika katika Shirika la Habari za Qur'ani la Kimataifa (IQNA).  Kitabu hicho chenye kurasa 210 kimechapishwa na Tume ya Kiislamu ya Haki za Binadamu yenye makao yake London na kinaelekezea bayana kuhusu nafasi ya taasisi za kifikra za Marekani katika kueneza na kuchochea fikra za chuki dhidi ya Uislamu ndani ya serikali ya Marekani na katika uga wa kimataifa.

Saeed Khan mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Wayne State nchini Marekani amekitaja kitabu hicho kuwa chenye uchambuzi wa kiwango cha juu.

3909159

captcha