IQNA

Watoto,vijana wengi Algeria wajisajili kushiriki darsa za Qur'ani

15:14 - August 15, 2019
Habari ID: 3472084
TEHRAN (IQNA) – Idadi kubwa ya vijana na watoto nchini Algeria wamejisajili kushiriki katika darsa za Qur'ani zinazofanyika katika misikiti na vituo vya Qur'ani katika mkowa wa Constantine kaskazini mashari mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa, vijana na watoto wengi wamevutiwa na masomo hayo ya Qur'ani ambayo yanafanyika katika msimu wa joto, wakati ambao shule za huwa zimefungwa nchini humo.

Familia nyingi zinaamini kuwa, watoto hawapati fursa ya kusoma Qur'ani wakati shule zikiwa zimefunguliwa kwa hivyo msimu wa joto hutumiwa kama fursa ya kujifunza Qur'ani na kuhifadhi aya zake.

Kwa mfano Abdul Rahman Wasim, 14, anasema anashiriki katika kozi ya kuhifadhi Surah al-Baqara na anaongeza kuwa, hangeweza kujisajili katika kozi hiyo wakati masomo ya shule yakiendelea hivyo ametumia fursa ya likizo ya msimu wa joto kuhifadhi Qur'ani.

Kozi hizo zinajikita Zaidi katika kusoma na kuhifadhi Qur'ani na pia Hadithi za Mtume SAW pamoja na umuhimu wa Swala.

Algeria ni nchi ya Afrika Kaskazini na asilimia 99 ya wakazi wake ni Waislamu.

3834892  

captcha