IQNA

Bi. Marziyah Hashemi

Kilichonivutia katika Uislamu ni Tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu)

13:03 - May 21, 2019
Habari ID: 3471967
TEHRAN (IQNA) – Mmarekani-Muirani mwenye asili ya Afrika, Bi. Marzieh Hashemi anasema msingi wa Tauhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu) ni nukta ambayo ilimvutia katika Uislamu na kumfanya asilimu.

Akizungumza Jumatatu usiku katika hafla malumu ya 'Walioweza Kupata Njia ya Haki' katika Maonyesho ya 27 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Tehran, Bi. Hashemi ambaye ni mwandishi habari na mtangazaji maarufu katika Televisheni ya Press TV, anasema alizaliwa katika familia ya Kikristo nchini Marekani na kwa msingi huo amekuwa akimuamini Mwenyezi Mungu tokea utotoni.

Bi. Hashemi, ambaye alikuwa akiitwa Melanie Franklin kabla ya kusilimu, anasema ilikuwa vigumu kwake kukubali msingi wa Utatu katika Ukristo na hivyo alivutiwa na msingi wa Tauhidi katika Uislamu.

Halikadhalika Bi. Hashemi anasema mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyopata ushindi katika mwaka 1979 wakati akiwa mwanafunzi katika chuo kikuu nchini Marekani na hivyo mapinduzi hayo yaliyoongozwa na Imam Khomeini yalikuwa pia sababu nyingine iliyomfanya avutiwe na Uislamu.

Bi. Hashemi ambaye baada ya kusilimu aliolewa na mwanafunzi mwenzake kutoka Iran anasema alichukua muda wa miaka miwili kufanya utafiti kuhusu Uislamu.

3813338

captcha