IQNA

Waislamu wanateswa na kudhalilishwa katika magereza ya Australia

17:41 - October 16, 2017
Habari ID: 3471219
TEHRAN (IQNA)-Waislamu katika magereza ya Australia wanakabiliwa na mateso, udhalilishaji na ukandamizaji mikononi mwa maafisa wa gereza.
Waislamu wanateswa na kudhalilishwa katika magereza ya AustraliaBaraza la Kiislamu katika Jimbo la Queensland limesema limepokea taarifa kuwa Waislamu katika Gereza ya Brisbane wanateswa na kudhalilishwa na maafisa wa Gereza la Arthur Gorrie ambalo ni kubwa zaidi jimboni humo.

Inadokezwa kuwa, mara kadhaa wafungwa wasiokuwa Waislamu wamechochewa na maafisa wa gereza kuwapiga wafungwa Waislamu.

Aidha wakati moja mkuu wa gereza hilo aliingia katika seli na alipowapata Waislamu wanaswali sala ya jamaa alidia kuwa wanahusika na hujuma za kigaidi. Aidha katika tukio hilo aliwatisah Waislamu kuwa atachukua hatua kali dhidi yao wakiendelea kuswali pamoja.

Jesse Price mwenye umri wa miaka 21 na aliyekuwa mfungwa katika gereza ya Upper Coomera, katika jimbo hilo la Queensland na aliyesilimu mwezi Oktoba ndiye mfungwa pekee aliye na ujasiri wa kuzungumza kuhusu ukandamizaki wa Waislamu magerezani. Anasema anawasiliana na Waisalmu wambao wanaendelea kuteswa gerezani. Msemaji wa Baraza la Kiislamu la Queensland Ali Qadri amesema Waisalmu wanakumbwa na matatizo gerezani ikiwa ni pamoja na kukosa chakula halali.

3464180

captcha